Azam FC 4-0 Fountain Gate FC ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo Aprili 12, 2026 Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni hatua ya 16 bora.
Matajiri wa Dar waligawa mchezo kwa kila dakika 45 wakipata magoli mawili ambapo walikwenda mapumziko ubao ukisoma Azam FC 2-0 Fountain Gate na kipindi cha pili wakaongeza magoli mawili.
Magoli ya Azam FC yamefungwa na Jephte Kitambala dakika ya 15, Abah Abel dakika ya 21, Asharafu Kibeku dakika ya 81 na kamba ya nne ikifungwa na Alobogast Kyobya dakika ya 90.
Matokeo haya Azam FC inatinga hatua ya robo fainali huku Fountain Gate ikifungashiwa virago bila kupata goli la kufutia machozi.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.