HT: Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC, NBC Premier League, Uwanja wa CCM Kirumba, Machi 19,2026.
Simba SC walianza kufunga dakika ya 33 ni Anicent Oura alifungua ukurasa na goli hilo lilidumu kwa dakika 3 kabla wenyeji kujaza mpira kimiani.
James Mwashinga alifunga goli la usawa dakika ya 36 ya mchezo na kuwanyanyua mashabiki wa Pamba Jiji FC.
Huu ni mchezo wa pili mfululizo kwa Simba SC kuanza kufunga ndani ya dakikachache goli linarudishwa kama ilivyokuwa mchezo uliopita dhidi ya Singida Black Stars.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.