FT: Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC

PAMBA Jiji FC 1-1 Simba SC ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Uwanja wa Kirumba, leo Machi 19,2026.

Alianza Anicent Oura alianza kufunga goli kwa Simba SC dakika ya 33 na dakika ya 36 James alifunga goli kwa upande wa Pamba Jiji FC.

Licha ya mnyama kuanza kutangulia kufunga kwenye mchezo alikwama kulinda ushindi huo na makosa ya safu ya ulinzi ikawa ni faida kwa Pamba Jiji FC ya Mwanza kupata goli la usawa dakika 3 baada ya kufungwa.

Simba SC inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo na Pamba Jiji FC nafasi ya 5 pointi 25.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.