YANGA WAIACHA MBALI SIMBA KWENYE MABAO NA POINTI

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic wamewaacha mbali watani zao wa jadi kwenye tofauti ya pointi na idadi ya mabao ya kufunga.

Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex Februari Mosi 2o25 Yanga imefikisha pointi 42 ikiishusha Simba nafasi ya kwanza.

Ni tofauti ya pointi mbili kwa kuwa Simba ina pointi 40 baada ya kucheza mechi 15 huku Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 16.

Kwenye idadi ya mabao Yanga ni namba moja kwa timu zenye mabao mengi ambayo ni 36 wakiwaacha Simba kwa tofauti ya mabao matano ndani ya msimu wa 2024/25.

Simba ni mabao 31 wamefunga huku Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao 36 na kwenye vinara kutoka timu hizo wote wakali wao wametupia mabao 7, Jean Ahoua wa Simba na Clement Mzize wa Yanga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.