Kipa namba mbili wa Simba, Ally Salim ameanzia benchi kwenye mchezo dhidi ya Tabora United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Salim alianza katika mchezo uliopita dhidi ya Kilimanjaro Wonders ambao ulikuwa ni CRDB Federation Cup.
Kikosi kipo namna hii:- Mousa Camara, Shomari Kapombe, Zimbwe Jr, Hamza Jr, Che Malone.
Yusuph Kagoma, Kibu Dennis, Fabrice Ngoma, Leonel Ateba, Jean Ahoua na Mpanzu.
Kikosi cha akiba ni Ally, Nouma, Chamou, Mzamiru, Mavambo, Chasambi, Mutale, Mukwala, Mashaka na Alexander.
Ikumbukwe kwamba kwenye msimamo Simba ni namba mbili ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 15 vinara ni Yanga wenye pointi 42 baada ya kucheza mechi 16 ndani ya msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.