NDANI ya Februari Simba itakuwa na mechi za tano za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni ligi namba nne kwa ubora ikiwa inadhaminiwa na NBC.
Ni dakika 450 za msako wa pointi 15 ndani ya ligi ambapo kwa sasa Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 15 vinara ni Yanga wenye pointi 42 baada ya kucheza mechi 16.
Hii hapa ratiba:-
Tabora United v Simba, Februari 2 2025 ugenini
Fountain Gate v Simba, Februari 6 2025, ugenini.
Simba v Tanzania Prisons, Februari 11 2025, nyumbani.
Simba v Dodoma Jiji, Februari 15 2025, nyumbani
Simba v Azam FC, Februari 24 2025, nyumbani.
Mechi tatu ambazo ni dakika 270 Simba itakuwa nyumbani, mbili ambazo ni dakika 180 watakuwa ugenini katika msako wa pointi ndani ya dakika 90.