MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na beki ya NBC Yanga wamekomba pointi tatu muhimu na kuishusha Simba nafasi ya kwanza baada ya kufikisha jumla ya pointi 24 huku Simba wakiwa na pointi 40 nafasi ya pili kwenye msimamo.
Yanga imecheza mechi 16 na Simba imecheza mechi 15 mchezo wake wa 16 unatarajiwa kuchezwa Februari 2 itakuwa dhidi ya Tabora United.
Kwenye mchezo wa Februari Mosi 2025 Clement Mzize alianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 33 akitumia pasi ya kiungo mshambuliaji Aziz Ki ambaye alitoa kwa mguu wake wa kushoto.
Dakika mbili mbele Yanga walipata penati ni Aziz Ki alipewa jukumu la kupiga penalti hiyo lakini alikosa baada ya mlinda mlango Ramadhan Chalamanda kuikoa.
Dakika 45 zilikamilika Yanga ikiwa mbele kwa bao 1-0 Kagera Sugar kwenye mchezo wa mzunguko wa pili na mwamuzi Nassoro Mwinchui akiwa pilato wa mchezo huo.
Kipindi cha pili, Yanga walifunga mabao matatu kupitia kwa Mudathir Yahya dakika ya 59, bao la pili likafungwa na Pacome kwa pigo la penati dakika ya 77 likiwa ni bao la tatu kwenye mchezo na bao la tatu kipindi cha pili lilifungwa na Kennedy Musonda dakika ya 86.
Yanga imeshinda nje ndani mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Kaitaba na mzunguko wa pili ni mabao 4-0 Uwanja wa KMC, Complex.