TABORA UNITED YAPOTEZA,SIMBA YAISHUSHA YANGA

IKIWA ugenini dhidi ya Tabora United Simba imepata ushindi wa mabao 3-0 baada ya dakika 90 kukamilika.

Leonel Ateba alifunga mabao mawili dakika ya 12 na 34 kwa mkwaju wa penalti baada ya Mpanzu kuchezewa faulo na beki wa Tabora United ndani ya 18.

Ateba anafikisha mabao 7 sawa na kiungo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Bao la tatu ni mali ya Shomari Kapombe beki wa kupanda na kushuka amefunga bao hilo dakika ya 66.

Simba inafikisha pointi 43 inarejea nafasi ya kwanza ikiishusha Yanga yenye pointi 42 zote zimecheza mechi 16 ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.