MCHEZAJI bora kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex, Maxi Nzengeli amesema kuwa mwalimu wa timu hiyo anahitaji kujituma zaidi katika mechi za ushindani.
Katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex Februari Mosi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 4-0 Kagera Sugar ambapo Maxi alianzia benchi aliingia dakika ya 70.
Kwenye mchezo huo alitoa pasi moja ya bao dakika ya 86 likifungwa na Kenned Musonda ambaye naye alianzia benchi ni baada ya kuanzisha kona ya haraka kwenye mchezo huo.
Maxi baada ya dakika 90 alichaguliwa kuwa mchezaji bora huku akiweka wazi kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa taratibu anarejea kwenye ubora wake.
“Ninamshukuru Mungu ni mchezo wangu wa pili sasa ninacheza na kufanya vizuri, mwalimu amekuwa akipenda kuona timu inapata matokeo na kujituma kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo nina amini kwamba tutaendelea kufanya vizuri.”
Kwenye msimamo wa ligi Yanga ni namba mbili ikiwa na pointi 42 baada ya kucheza mechi 16 vinara ni Simba wenye pointi 43 tofauti ya pointi moja ila michezo wote ni sawa.
Maxi ni mabao matatu kwenye ligi akiwa ametoa jumla ya pasi tatu za mabao msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.