BEKI YANGA AMEPANIA JAMBO HILI

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Ibrahim Bacca ametangaza vita yake dhidi ya kinara wa utupiaji Bongo, Suleman Mwalimu wa Fountain Gate.

Mwalimu katupia jumla ya mabao sita ndani ya ligi akiwa kinara kwenye eneo hilo anafuatiwa na Edger William mwenye mabao manne naye yupo ndani ya kikosi cha Fountain Gate.

Bacca ndani ya ligi ametupia mabao mawili msimu wa 2024/25 bao la kwanza alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Sokoine Mbeya amebainisha kuwa anahitaji tuzo ya ufungaji bora.

Nyota huyo ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga kwenye eneo la ulinzi amesema kuwa Mwalimu ajiandae kupisha nafasi hiyo kutokana na mpango kazi mkubwa wa kuendelea kufunga zaidi.

“Mwalimu yule ambaye anaongoza namtumia salamu ajiandae kuondoka eneo hilo kwa kuwa sasa ninarejea kwenye ubora na malengo ni kuona ninafanikiwa kufunga mabao mengi zaidi na sasa nimerudi awali sikufunga sasa nitafunga mechi zinazofuata.”

Yanga Oktoba 30 2024 ilishuhudia ubao ukisoma Singida Black Stars 0-1 Yanga kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar bao likifungwa na Pacome.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.