FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mashujaa wanahitaji pointi tatu muhimu.
Simba Novemba Mosi 2024 itakuwa ugenini Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kusaka pointi tatu dhidi ya Mashujaa ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Fountain Gate.
Fadlu amesema; “Ni mchezo muhimu kwetu na tunatambua ushindani utakuwa mkubwa jambo ambalo tunahitaji ni pointi tatu muhimu.”
Mchezo uliopita Simba ilishuhudia ubao wa Uwanja wa KMC, Mwenge ukisoma Simba 3-0 Namungo na Shomari Kapombe alifunga bao moja na kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo.
Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya 3 na pointi 19 baada ya kucheza mechi 8 inakutana na Mashujaa yenye pointi 13 nafasi ya 6. Ikumbukwe kwamba Mashujaa wazee wa mapigo na mwendo hesabu zao ni kuvuna pointi tatu pia za Simba.