>

RONALDO AMKOSOA TEN HAG NA KUSEMA MAN UTD LAZIMA ‘IJENGE UPYA KILA KITU’

Cristiano Ronaldo amemkosoa meneja wa Manchester United Erik ten Hag na kusema klabu hiyo lazima “ijenge upya kila kitu” ili kuwania tuzo kubwa zaidi za soka tena.

Mkufunzi huyo wa Uholanzi yuko chini ya shinikizo baada ya United kumaliza katika nafasi ya nane msimu uliopita – chini kabisa katika historia ya Ligi Kuu – na kushindwa mara mbili katika mechi tatu za mwanzo mwanzoni mwa kampeni hii.

Na Ronaldo, ambaye aliichezea klabu hiyo mara mbili kabla ya kwenda Al-Nassr ya Saudi Arabia, alitilia shaka mawazo ya Ten Hag.

“Kocha anasema hawawezi kushindana katika[Premier] League na Ligi ya Mabingwa,” aliambia podikasti ya Rio Ferdinand Presents. ambayo inatoka Alhamisi.

“Kama kocha wa Manchester United, huwezi kusema kwamba hutapambana kushinda ligi au Ligi ya Mabingwa.

“Kiakili [unaweza] kusema labda hatuna uwezo huo, lakini siwezi kusema hivyo. Tutajaribu, lazima ujaribu.

“Ninachotamani kwa Manchester [United], ndicho ninachotamani kwangu – [kuwa] timu bora wanayoweza.

“Naipenda klabu hiyo… mimi si mtu wa aina hiyo ambaye alisahau yaliyopita.”

Katika kipindi chake cha miaka sita cha kwanza akiwa United, Ronaldo alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Vikombe viwili vya Ligi na Kombe la FA – pamoja na Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa na Community Shield – kabla ya kuhamia Real Madrid mnamo 2009.