>

KIMATAIFA NI BALAA ZITO HUKO, HII HAPA RATIBA

KWENYE anga la kimataifa balaa ni zito kwa kuwa wikiendi itakuwa bize kwa wawakilishi wa Tanzania kupeperusha bendera uwanjani kusaka ushindi ndani ya dakika 90 za kazikazi uwanjani.

Ipo wazi kwamba ni Simba na Yanga hizi zipo anga la kimataifa baada ya Azam FC matajiri wa Dar na Coastal Union inayotumia Uwanja wa Mkwakwani, kwenye mechi za nyumbani kugotea katika hatua ya awali ambapo walicheza mechi mbili wakitumia dakika 180 kimataifa.

Jumamosi Septemba 14  2024 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi atakuwa nchini Ethiopia ikisaka ushindi mbele ya CBE SA wataanza ugenini.

Mechi hiyo itapigwa saa 9:00 Alasiri na itakuwa mbashara AzamSports2HD hivyo burudani kwa mashabiki wa Tanzania itaendelea palepale wakiwa Bongo na wale watakaokwea pipa watakuwa uwanjani.

Jumapili Septemba 15 2024 Simba  inayonolewa na Fadlu Davids itakuwa nchini Libya kumenyana na Al Ahly Tripoli mchezo wa Kombe la Shirikisho. Ni saa 2:00 usiku mchezo huo utachezwa na utakuwa live AzamSports1 HD

Pia Gor Mahia wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya  mabingwa wa Afrika Al Ahly wenye tabia ya kubadilika kwenye anga la kimataifa itakuwa Septemba 15 saa 9: 00 alasiri itakuwa mubashara Azam TV.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka.