MWAMBA SAIDO ATAJWA COASTAL UNION

MKALI wa mabao ndani ya kikosi cha Simba msimu wa 2023/24 Saido Ntibanzokiza anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Coastal Union ya Tanga.
Nyota huyo akiwa na kikosi cha Simba msimu wa 2023/24 ni mabao 11 alifunga akiwa namba moja kwenye chati ya wafungaji wa Simba ambapo kinara ni Aziz Ki wa Yanga mwenye mabao 21.
Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo hajaongeza dili jipya ndani ya Simba hivyo huenda akajiunga na Coastal Union ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho msimu wa 2024/25 baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.
Simba pia itashiriki Kombe la Shirikikisho Afrika kwa kuwa iligotea nafasi ya tatu, Yanga na Azam FC hizi zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.