LEO NI LEO KWA MABINGWA YANGA

SIKU iliyokuwa inasubiriwa na Wanachama pamoja na viongozi wa Yanga imewadia ambayo ni leo Juni 9 2024 ambapo kutakuwa na mkutano mkuu.

Yanga  watafanya Mkutano Mkuu wa Mwaka katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa kuelekea kwenye mkutano huo ambao utakuwa wa kipekee huku baadhi ya matawi mengine yakiongezeka kwa kukidhi vigezo vya kushiriki mkutano huo.

Ikumbukwe kwamba Kamati ya Utendaji ya Yanga  chini ya Hersi Said Juni 7 2024 ilifanya kikao maalumu cha maandalizi ya Mkutano mkuu wa Wanachama (Annual General Meeting – AGM) katika ukumbi wa Urban By City Blue, Masaki Jijini Dar hivyo kwa asilimia kubwa mipango ipo vizuri.

Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi imemaliza msimu ikitwaa taji la Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya kwanza na pointi 80 ilitwaa pia taji la CRDB Federation Cup mbele ya Azam FC kwenye fainali na walitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.