ALICHOKISEMA RAIS WA YANGA, INJINIA HERSI SAID KWENYE MKUTANO MKUU

“Tulifanikiwa kurejea hatua ya makundi ligi ya Mabingwa AFRIKA baada ya miaka 25. Watu wengi walidhani kuwa hatutaweza kufika hatua ya robo fainali kwa sababu tulikuwa kwenye kundi gumu sana. Lakini tukawashangaza wale waliotukatia tamaa.

Tulifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kutolewa kwa matuta na Bingwa wa AFL na kigogo wa soka AFRIKA KUSINI, Mamelodi Sundowns. Hata hivyo katika mchezo tulifunga bao halali ambalo Rais wa Soka AFRIKA, Dr.Patrice Motsepe amenukuliwa akisema kuwa lilikuwa goli halali”

“Klabu yetu inahitajika kujengeka kiuchumi. Kazi yetu kama viongozi ni kuhakikisha tunapata wadhamini ambaye atasaidia na mfadhili wetu GSM. Lakini mashabiki wetu pia wanao mchango mkubwa kwa kuhakikisha kuwa kupitia ada za Wanachama tunapata mapato ya kuendesha klabu yetu”

“Naawahidi mashabiki na Wanachama tutafanya usajili mkubwa sana msimu ujao. Msimu ujao tutafanya mambo makubwa kuanzia ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Tutafanya Pre season nzuri, tumeshapata mialiko maeneo mbalimbali ikiwemo AFRIKA KUSINI, Kaizer Chiefs wametoa mwaliko na Mh.Raila Odinga ametuomba tuungane nao kwenye uzinduzi wa Uwanja wao huko Kisumu pamoja na nchi moja ya ulaya”

“Leo tupo na Mheshimiwa Mchengerwa, na tayari amepokea maombi yetu kuhusu mchakato wetu wa ujenzi wa Uwanja wetu hapa Jangwani. Jambo la kheri ni kuwa amejumuika nasi moja kwa moja akitokea Tabora. Mradi wetu huu wa ujenzi wa Uwanja tayari upo ofisini kwake na analifanyia kazi.

Mdhamini na mfadhili wetu GSM yupo tayari kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja. Kwa bahati mbaya, GSM hajawahi kutoa ahadi hewa. Hivyo niwaahidi wanachama na mashabiki wetu kuwa mchakato wetu upo tayari kuanza kwa kuzingatia mradi wa mto Msimbazi” amesema Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said