>

WAZIRI MCHENGERWA: HONGERA INJINIA HERSI KWA KUFANYA YANGA KUWA YA KISASA

“Nawashukuru sana Young Africans SC kwa kunialika kwenye mkutano wenu huu mkuu. Ni heshima kujumuika nanyi ikiwa nyie ni Klabu yenye mafanikio makubwa sana. Nafikisha salamu za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa chachu kwenye maendeleo ya soka nchi hii” Mgeni Maalum Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
“Mafanikio ya leo ya Yanga, kuna watu walifanya kazi kubwa kuhakikisha klabu hii inatulia. Utulivu wa Yanga ndio maendeleo ya soka letu. Mafanikio ya Yanga leo ni kwa sababu ya Injinia Hersi na wenzake walifanya kazi kwa utulivu na weledi mkubwa. Hongera sana Injinia Hersi kwa kufanya Klabu ya kisasa zaidi. Uwekezaji uliofanywa kwenye klabu hii imekuwa chachu ya maendeleo ya soka Tanzania.” Amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa kwenye Mkutano Mkuu wa YANGA