Home Sports WATAKAOKUTANA ROBO FAINALI CRDB FEDERATION CUP HADHARANI

WATAKAOKUTANA ROBO FAINALI CRDB FEDERATION CUP HADHARANI

CRDB Bank Federation Cup kwa sasa ni hatua ya robo fainali ambapo kila timu imetambua ilipogotea baada ya dakika 90 kwenye msako wa ushindi katika hatua ya 16 bora.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ambao ni Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi wamepenya katika hatua ya robo fainali walipata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji.

Leo saa 6:00 Aprili 17  droo ya robo fainali itafanyika na kuruka mubashara kupitia AzamSports3HD.

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Namungo FC, Geita Gold FC, Tabora United, Coastal Union, Ihefu SC, AzamFC, Mashujaa FC na Yanga.

Hivyo kila timu nakwenda kutambua itakutana na nani kwenye hatua ya robo fainali kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Previous articleDORTMUND YATINGA NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Next articleWAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU HAWA HAPA