Home Sports AZAM FC WAIKANDA NAMUNGO NYUMBANI

AZAM FC WAIKANDA NAMUNGO NYUMBANI

USHINDI waliopata Azam FC kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 0-2 Azam FC unawaongezea nguvu kubaki nafasi ya pili ndani ya msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Matajiri wa Dar, Azam FC wameikanda Namungo ikiwa nyumbani mzunguko wa pili na kulipa kisasi cha kufungwa mzunguko wa kwanza walipokuwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao yote ya Azam FC yalifungwa kipindi cha pili na Kipre Junior ilikuwa dakika ya 62 na 84 hivyo Azam FC imekomba pointi tatu ugenini.

Nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 22 ikiwa na pointi 50 nafasi ya tatu ni Simba wenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 vinara ni Yanga wenye pointi 55.

Previous articleKasino ya Fruit Salad 100 Ushindi 95.06%
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE CHAMPIONI JUMATATU