Home Uncategorized KITAWAKA LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA ARSENAL VS BAYERN MÚNICH, REAL MADRID...

KITAWAKA LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA ARSENAL VS BAYERN MÚNICH, REAL MADRID VS MAN CITY

HOLOMICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea leo Aprili 9, 2024 kwa michezo miwili ya mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ambapo itamshuhudia Harry Kane akirejea Kaskazini mwa Jiji la London kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka Tottenham na kujiunga na miamba ya Ujerumani, Bayern Munich.

Kane anatarajiwa kuwa mwiba mkali kwa wenyeji, Arsenal dhidi ya Waajiri wake Bayern Munich ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kiushindani baina ya timu hizo yangu kipigo cha 5-1 cha Washika Mitutu dhidi ya Bayern mnamo Machi 7, 2017.

Arsenal ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England ipo kwenye kiwango bora sana kwa sasa tofauti na ilivyokuwa wakati inakubali vichapo vitatu mfululizo vya 5-1 (Machi 7, 2017), 5-1 (Februari 15, 2017) na 5-1 (Novemba 4, 2015) kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo ‘The Gunners’ wanakutana na Bayern Munich ambayo ipo ‘unga’ mno kwa sasa ambayo inatarajiwa kushindwa kutetea ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza baada ya misimu 11. Bayern ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga ikiwa alama 16 nyuma ya kinara Bayer Leverkusen ambaye anatarajiwa kutangazwa bingwa ikiwa ataibuka na ushindi dhidi ya Werder Bremen weekend hii.

Hii ni fursa kwa Arsenal kutumia mwenendo mbaya wa Bayern Munich kama daraja la kuivusha kwenda hatua ya nusu fainali na kuweka hai matumaini yake ya kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza kihistoria.

Mchezo wa leo pia utamshuhudia winga wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry akirejea Emirates Stadium akiwa na uzi wa Bayern huku akitarajiwa kuleta madhara kwa nahodha wake wa zamani wakati akiwa Arsenal, Mikel Arteta ambaye ndiye kocha wa Washika Mitutu kwa sasa.

22:00 Arsenal vs Bayern Múnich
🏟️ Emirates

22:00 Real Madrid vs Manchester City
🏟️ Santiago Bernabéu

Previous articleMOTO WA YANGA KIMATAIFA HAUZIMI/MAMELODI WALIKUTANA NA BALAA
Next articleFT: MASHUJAA 1-1 SIMBA, LAKE TANGANYIKA, (6-5)