Home Sports FT: MASHUJAA 1-1 SIMBA, LAKE TANGANYIKA, (6-5)

FT: MASHUJAA 1-1 SIMBA, LAKE TANGANYIKA, (6-5)

CRDB Federation Cup.

Mashujaa wanaifunagshia virago Simba kwenye CRDB Federation Cup kwa ushindi wa penalti 6-5 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Simba haina bahati mbele ya Mashujaa kwa kuwa iliwahi kutolewa walipokutana kwenye mashindano hayo hivyo kisasi cha ushindi kwenye ligi kimelipwa mazima katika raundi ya nne.

Mashujaa 1-1 Simba

Lusajo dakika ya 5 kipindi cha kwanza kwa Mashujaa

Fred Michael dakika ya 54 kwa Simba

Mashujaa hawataki unyonge mbele ya Mnyama Simba kazi imeanza mapema dakika ya 5 kwa bao la kuongoza kutoka kwa Relliat Lusajo.

Ni pigo la kona limewapa faida Mashujaa baada ya harakati za ukuta wa Simba kupambana kuokoa Habari.

Mashujaa wameongeza nguvu kubwa eneo la ulinzi huku Simba wakiwa hawana utulivu kila wanapokuwa ndani ya eneo ya 18 kwa Mashujaa FC wazee wa mapigo na mwendo.

Nyota Said Juma dakika ya 45 ameonyeshwa kadi ya njano kutokana na kuwa na kadi ya njano mapema dakika ya 36 hivyo kadi mbili zimemfanya aonyeshwe kadi nyekundu.

Previous articleKITAWAKA LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA ARSENAL VS BAYERN MÚNICH, REAL MADRID VS MAN CITY
Next articleRATIBA YA MICHEZO ILIYOSALIA YA LIGI KUU