Home Sports YANGA HAWANA HOFU KIMATAIFA

YANGA HAWANA HOFU KIMATAIFA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns hawana hofu kwa kuwa wanaamini kwenye ubora walionao.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa tatu usiku kwa kila timu kupambana kupata ushindi kuongeza nguvu kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo ni hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo kuchezwa na Yanga kuwtambua wapinzani hao kwenye anga la kimataifa.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua ukubwa wa mchezo huo katika mechi za kimataifa jambo ambalo linawafanya wawe tayari kuelekea kwenye mchezo huo mgumu.

Tunatambua ni mchezo mgumu lakini ni mchezo mkubwa tumejiweka sawa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo huu na ugumu uliopo kwenye kupata matokeo kimataifa tupo tayari tutapambana kupata ushindi hilo lipo wazi,”.

Previous articleUnashida TV, Simujanja na Maokoto Kibao Ukicheza Super Heli Kasino
Next articleWAARABU WA MISRI KUKUTANA NA MTEGO WA SIMBA