Home Uncategorized HIZI HAPA HESABU ZA AZAM FC

HIZI HAPA HESABU ZA AZAM FC

 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi huwa mpango kazi wao ni kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.

Hasheem Ibwe Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa ambacho wanakihitaji ni kuwa kwenye kasi ileile waliyokuwa nayo kwenye ligi kwa kupata ushindi na burudani kuwapa mashabiki zao.

Ipo wazi kwamba Azam FC ilikwama kutwaa taji la Mapinduzi 2024 ambalo ni mali ya Mlandege.

“Ushindani ni mkubwa na hesabu zetu ni kuona kwamba tunakuwa kwenye mwendo mzuri inawezekana na tutafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa uliopo.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani kila kitu kinawezekana na wao wamekuwa chachu kwenye upatikanaji wa matokeo,’ amesema Ibwe.

Azam FC ni vinara wa msimamo kwenye ligi wakiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 wakiwa na pointi 31 na kinara wa utupiaji ni Feisal Salum mwenye mabao 8.

Previous articleAZIZ KI NA DIARRA ISHU YAO KUONDOKA YANGA TAMKO LATOLEWA
Next articleAMETAJA SIKU YA NYOTA SIMBA KUTUA