AZIZ KI NA DIARRA ISHU YAO KUONDOKA YANGA TAMKO LATOLEWA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa uwezo wa wachezaji wao kwenye mechi za kitaifa ni kimataifa ni mkubwa jambo ambalo linawafanya wawe kwenye hesabu za kusajili na timu nyingine. Miongoni mwa nyota ambao wanatazamwa kwa ukaribu ni pamoja na Aziz KI ambaye ni kiungo mwenye mabao 10 pamoja na kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra. Nyota hao kwa sasa wapo kwenye majukumu ya timu Taifa, Afcon kila mmoja akipambania majukumu yake.