Home International NSUE ANAPIGA HESABU ZA UFUNGAJI BORA AFCON

NSUE ANAPIGA HESABU ZA UFUNGAJI BORA AFCON

MSHAMBULIAJI wa Equatorial Guinea, Emilio Nsue ametamba kuwa sasa anatamani kuwa mfungaji bora wa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) ikiwa ni baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika mchezo wao dhidi ya Guinea Bissau.

Nsue Alhamisi aliweka rekodi ya kipekee katika mashindano ya AFCON yanayoendelea nchini Ivory Coast baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao hayo katika mashindano hayo na kuiongoza timu yake kushinda mabao 4-2 mbele ya wapinzani wao hao.

Hat trick hiyo ya Nsue ambayo aliifunga dakika za 21, 51, 61, pia inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao hayo katika AFCON tangu Mmorocco, Soufiane Alloudi afunge mwaka 2008.

Nsue, 34, amesema: “Ninajisikia vizuri sana na ninafuraha kucheza AFCON yangu hii ya tatu. Kufunga mabao matatu inanipa ujasiri na nina matumaini nitafunga zaidi na hata kuwa mfungaji bora wa mashindano.

“Ninajivunia pafomansi ya wachezaji wenzangu. Ilikuwa mechi nzuri hasa katika kipindi cha pili, hata hivyo tunatakiwa kuimarika katika baadhi ya maeneo.”

Previous articleMWAMBA ALIYETAKIWA YANGA KAMWAGA WINO HUKU
Next articleTAIFA STARS KWENYE MIKONO YA MAKOCHA HAWA