Home Uncategorized MWAMBA ALIYETAKIWA YANGA KAMWAGA WINO HUKU

MWAMBA ALIYETAKIWA YANGA KAMWAGA WINO HUKU

SIMON Msuva winga mzawa ambaye yupo na timu ya Tanzania, Taifa Stars, Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) amesaini dili la miaka miwili Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini.

Nyota huyo aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Yanga ambapo alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za kurejeshwa hapo kwa mara nyingine tena.

Taarifa zimeeleza kuwa mchezaji huyo amesaini dili la mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo hivyo hatajiunga na Yanga wakati huu mpaka wakati ujao ikiwa watafikia makubaliano mazuri.

Timu ya Taifa ya Tanzania inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili hatua ya makundi wakiwa kundi F itakuwa dhidi ya Zambia.

Januari 21 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa baada ya ule wa awali Januari 17 kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco ambapo Msuva anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye kazi hiyo.

Kwa sasa alikuwa mchezaji huru baada ya kutokuwa na timu kwa kuwa ile aliyokuwa awali ilisitisha mkataba wake.

Previous articleAMEIGOMEA SIMBA KIUNGO HUYU WA KAZI
Next articleNSUE ANAPIGA HESABU ZA UFUNGAJI BORA AFCON