Home International TAIFA STARS IMEANZA KWA MWENDO HUU, KAZI BADO INAENDELEA

TAIFA STARS IMEANZA KWA MWENDO HUU, KAZI BADO INAENDELEA

BALAA lilikuwa zito kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stara dakika ya 70 baada ya Novatus Dismas kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa mbili za njano.

Wakati anatoka Tanzania ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Morocco ambapo bao lilipachikwa dakika ya 29 na Ghanem

Mabao mawili yalifungwa ndani ya dakika mbili ilikuwa dakika ya 76 na 78 katika mchezo wa Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON).

Aziz Eddine na Youssef En-nesyn hawa walimtungua kipa wa Stars, Aishi Manula ambaye alikuwa langoni.

Nahodha Mbwana Samatta hakukomba dakika zote 90 za mchezo nafasi yake ilichukuliwa na Fei Toto.

Novatus amesema kuwa hakumgusa mchezaji faulo ya pili iliyompa kadi ya njano.

Kazi bado inaendelea ambapo ikiwa kundi F mchezo ujao ni dhidi ya Zambia iliyogawana pointi mojamoja na DR Congo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Januari 21.

Previous articleHIVI HAPA VYUMA VIPYA SIMBA NA YANGA
Next articleAZAM FC WAMESHUSHA KITASA CHA KAZI