MAPINDUZI YAFANYIKE MAPINDUZI YA KWELI

WAKATI mwingine kwa sasa kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 ambapo kila timu shiriki inafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi. Hakuna ambaye hapendi kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ambao atacheza hivyo kwa sasa ni muhimu kupata ushindi. Ukweli ni kwamba wachezaji wamepata nafasi kwenye mashindano haya ambayo ni ya heshima na kila mmoja ana kazi ya…

Read More

SIMBA YATAJA SABABU YA KUTUNGULIWA NA MLANDEGE

GADIEL Michael, nahodha wa Simba kwenye kikosi kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi ameweka wazi kuwa sababu zilizofanya wakapoteza mchezo wa kwanza ni kushindwa kutumia nafasi. Ikiwa Uwanja wa Amaan, ilishuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Mlandege baada ya dakika 90 kukamilika. Ikumbukwe kwama Simba walikuwa ni mabingwa watetezi wamemaliza mwendo katika hatua hiyo wakianza kutunguliwa mchezo wao…

Read More

SIMBA YATUNGULIWA KOCHA MPYA AKISHUHUDIA

KOCHA Mkuu, Juma Mgunda akiwa amefanya mabadiliko makubwa kikosi cha kwanza kwa kumuazisha Beno Kakolanya langoni huku nahodha akiwa ni Gadiel Michael alionja joto ya jiwe.   Baada ya dakika 90 kukamilika Simba ambao ni mabingwa watetezi ubao ulisoma Simba 0-1Mlandege. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Abubakar Mwadin dakika ya 75 ya mchezo huo…

Read More

AZAM FC YATOSHANA NGUVU KOMBE LA MAPINDUZI

BAO la mapema kipindi cha kwanza kwa Azam FC lililofungwa na Ayoub Lyanga halikutosha kuipa pointi tatu timu hiyo. Ni kwenye Kombe la Mapinduzi ambalo linafanyika visiwani Zanzibar huku kila timu zikonyesha ushindani mkubwa. Baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Azam FC 1-1 Malindi FC na kufanya matajiri hao wa Dar kugawana pointi mojamoja….

Read More

MBRAZIL APEWA MIKOBA YA ZORAN SIMBA

RASMI Klabu ya Simba imemtangaza kocha Robertinho Oliveira kuwa kocha wao mkuu kupitia mkutano mkuu wa waandishi wa Habari uliofanyika leo Januari 3,2023. Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi ya Zoran Maki aliyebwaga manyanga hapo mwanzoni mwa msimu huu. Kocha huyo mpya ni raia wa Brazil na alikuwa anaifundisha Klabu ya Vipers ya Uganda ambayo ameachana…

Read More

PENALTI YAZUA UTATA FUNGUA MWAKA

JANUARI Mosi 2023 ilishuhudiwa penalti ambayo iliwafanya wachezaji wa Namungo FC kuonekana wakimlalamikia mwamuzi kutokana na mazingira ya penalti hiyo kuleta utata. Langoni kwa Namungo FC alikaa kipa mzawa Deogratius Munish, ‘Dida’ ambaye hakuwa na chaguo kutokana na mpigaji kupiga kwa umakini. Ni Maabad Maulid alifunga bao hilo akisawazisha bao lililofungwa na Ibrahim Mkoko nakuwafanya…

Read More

SIMBA KAMILI MAPINDUZI CUP,KAZI INAANZA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema maandalizi yapo sawa na wataonyesha ushindani. “Tupo tayari kwa ushindani na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi hivyo mashabiki wajue kwamba tutaonyesha ushindani. “Wachezaji wote ambao wapo kwenye kikosi cha Simba ni mali ya Simba na wanapaswa kutumikia timu yao. Januari 2,2023 kikosi cha Simba kiliibuka ndani…

Read More

MDAKA MISHALE AONGEZA DILI KUITUMIKA YANGA

WANANCHI wana uhakika wa kupata huduma ya Djigui Diarra ndani ya kikosi cha Yanga mpaka 2025. Chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameongeza dili jipya kuendelea kuitumikia timu hiyo. Mkataba wake wa mwanzo ulikuwa unagota ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa 2022/23. Mchezo wake uliopita kwenye ligi kuu langoni ilikuwa dhidi ya Mtibwa…

Read More

AZAM FC WANALITAKA KOMBE LA SIMBA

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa unalitaka Kombe la Mapinduzi hivyo hawatafanya makosa kwenye mashindano hayo. Ni Simba ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo la heshima ambalo limeanza Januari 2023, visiwani Zanzibar.  Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa lakini wamedhamiria kufanya kweli. “Hatuna utani raundi hii…

Read More