Home Sports SIMBA YATUNGULIWA KOCHA MPYA AKISHUHUDIA

SIMBA YATUNGULIWA KOCHA MPYA AKISHUHUDIA

KOCHA Mkuu, Juma Mgunda akiwa amefanya mabadiliko makubwa kikosi cha kwanza kwa kumuazisha Beno Kakolanya langoni huku nahodha akiwa ni Gadiel Michael alionja joto ya jiwe.

 

Baada ya dakika 90 kukamilika Simba ambao ni mabingwa watetezi ubao ulisoma Simba 0-1Mlandege.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Abubakar Mwadin dakika ya 75 ya mchezo huo huku kiungo wao Victor Akpan akifanya kazi ya kutibua mipango ya wapinzani wao.

Makosa ya mabeki kwenye kuokoa pigo la kona liliwapa tabu Simba na kuipa ushindi Mlandege ambayo imekuwa na mwendo mzuri kwa kuwa walipata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KVZ Januari Mosi 2023.

Mchezo ujao kwa Simba ni dhidi ya KVZ unaotarajiwa kuchezwa Januari 5,2023 saa 2:15 usiku.

Pia Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho Oliviera alikuwa jukwaani kushuhudia timu hiyo ikicheza na kupoteza.

Previous articleAZAM FC YATOSHANA NGUVU KOMBE LA MAPINDUZI
Next articleMBRAZIL: NAIPELEKA SIMBA FAINALI CAF, KISA YANGA, FEI TOTO AIPIGIA MAGOTI TFF