Home Uncategorized MDAKA MISHALE AONGEZA DILI KUITUMIKA YANGA

MDAKA MISHALE AONGEZA DILI KUITUMIKA YANGA

WANANCHI wana uhakika wa kupata huduma ya Djigui Diarra ndani ya kikosi cha Yanga mpaka 2025.

Chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameongeza dili jipya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mkataba wake wa mwanzo ulikuwa unagota ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa 2022/23.

Mchezo wake uliopita kwenye ligi kuu langoni ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Huo ulikuwa ni mchezo wa funga mwaka 2022 ambapo ubao wa Uwanja wa Manungu baada ya dakika 90 ulisoma Mtibwa Sugar 0-1 Yanga.

Bao la ushindi kwa Yanga lilipachikwa kimiani na mwamba Aziz KI ambaye amefikisha mabao manne ndani ya ligi.

Previous articleAZAM FC WANALITAKA KOMBE LA SIMBA
Next articleSIMBA KAMILI MAPINDUZI CUP,KAZI INAANZA