
MASHABIKI MNASTAHILI PONGEZI
MASHABIKI mnastahili pongezi kwa namna ambavyo mmekuwa bega kwa bega na wawakilishi wa Tanzania kwenye anga za kimataifa. Tunaona kwenye kila hatua mmekuwa pamoja na timu pale zinapofanya vizuri mnafurahi pamoja na pale zinaboporonga mnatoa ushauri kwa viongozi. Kuna mengi ya kujifunza kwa mechi za kimataifa ikiwa hata namna ya ushangiliaji pamoja na kutokata tamaa…