Home Sports MASHABIKI MNASTAHILI PONGEZI

MASHABIKI MNASTAHILI PONGEZI

MASHABIKI mnastahili pongezi kwa namna ambavyo mmekuwa bega kwa bega na wawakilishi wa Tanzania kwenye anga za kimataifa.

Tunaona kwenye kila hatua mmekuwa pamoja na timu pale zinapofanya vizuri mnafurahi pamoja na pale zinaboporonga mnatoa ushauri kwa viongozi.

Kuna mengi ya kujifunza kwa mechi za kimataifa ikiwa hata namna ya ushangiliaji pamoja na kutokata tamaa hata pale timu inapopoteza ikiwa uwanjani.

Wageni wamekuja Tanzania wakiwa na mashabiki wao kwenye mechi za kimataifa tumeona namna ambavyo wamekuwa wakitoa somo.

Licha ya kwamba ni wachache bado waliweza kuonyesha kitu cha kipekee na kuwafanya mashabiki wale ambao walikuwa wengi kuingia darasani.

Ipo wazi kwamba wao walianza kupenda mpira kisha timu ikafuata hivyo furaha yao ipo kwenye mpira pale unapochezwa hivyo wafungwe ama wasifungwe kazi yake ni kushangilia.

Imani yake ni wakati wao unakuja wa baadaye kushangilia na kuwa kwenye furaha katika mechi ambazo wanacheza.

Wachezaji wanatambua nguvu ya mashabiki ni kubwa lakini ikiwa itakuwa ipo na haitumiki inawapa hali ya unyonge licha ya kuwa wanakuwa uwanjani.

Kwenye kutafuta matokeo kila mmoja ni muhimu kujituma bila kuchoka na kuhakikisha kile ambacho kinatakiwa kinafanyika kwa wakati.

Makosa kwenye mechi ambazo zimepita ni muhimu kufanyiwa kazi ili kupata ushindi kwenye mechi zijazo, bado kazi inaendelea na mechi bado zinakuja.

Previous articleVIDEO:ILE MIHELA YA MAMA MIKONONI MWA YANGA
Next articleMwezi Februari Umekuwa Mtamu Sana kwa Washindi Hawa wa Meridianbet