Home Sports AZAM FC KAMILI KUIVAA SIMBA KWA MKAPA

AZAM FC KAMILI KUIVAA SIMBA KWA MKAPA

KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala kipo tayari kuelekea mchezo wake ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 21,Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Ni Azam FC waliitungua Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Prince Dube wanakutana kwa mara nyingine Uwanja wa Mkapa.

Wachezaji wote wa Azam FC wapo kamili gado kwa mchezo huo ikiwa ni pamoja na Dube mwenyewe, Idd Suleiman,Cleofance Mkanda,Idris Mbombo.

Ongala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wana imani wtapata matokeo chanya.

Previous articleYANGA KUJA NA MBINU TOFAUTI KUIKABILI TP MAZEMBE
Next articleVIDEO:CAF AFRICAN SCHOOLS FOOTBALL CHAMPIONSHIP ZONAL QUALIFIERS