Home Uncategorized TABORA UNITED WATANGAZIWA JAMBO HILI NA YANGA

TABORA UNITED WATANGAZIWA JAMBO HILI NA YANGA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa unazitaka pointi tatu za wapinzani wao Tabora United kuelekea mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ipo wazi kwamba Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 10 ina pointi 27 inakutana na Tabora United iliyo nafasi ya 12 na pointi 15.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua umuhimu wa pointi tatu kwenye mchezo wao pamoja na ushindani ambao wataupata.

Tunamchezo mgumu dhidi ya Tabora United ambao utakuwa na ushindani mkubwa lakini ambacho tunakihitaji ni pointi tatu muhimu kwa wapinzani wetu kwa kuwa wachezaji wapo tayari kupambania ushindi kwenye mchezo wetu.

Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani ambazo zitapatikana Uwanja wa CCM Kirumba hilo litawaongezea nguvu wachezaji kupambana dakika zote 90,” amesema Kamwe.

Previous articleSIMBA YAPOTEZA KARIAKOO DABI
Next articleMWENDELEZO WA LIGI KUU BARA UMAKINI UNAHITAJIKA