Home Uncategorized MWENDELEZO WA LIGI KUU BARA UMAKINI UNAHITAJIKA

MWENDELEZO WA LIGI KUU BARA UMAKINI UNAHITAJIKA

MWENDELEZO wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa kwanza unapaswa kuendelea kwa hesabu kubwa kwa timu ambazo zinashuka uwanjani kwa wakati huu.

Kila timu mpango kazi wake ni kupata matokeo hivyo kwa wale ambao hawajawa kwenye mwendo mzuri ni muda wa kufanya maboresho kwenye makosa yaliyopita.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri lakini kuna wachezaji wanaokwama kuonyesha viwango vyao katika mechi za ushindani.

Kwenye mapambano ya kusaka ushindi ni muhimu kuongeza nidhamu ndani ya uwanja nan je ya uwanja. Hilo litafanya kazi ziende kwa umakini na benchi la ufundi kupata fursa ya kuwatumia wachezaji wote ambao wapo katika kikosi.

Ikiwa wapo watakaokuwa wanakwenda tofauti kwenye maandalizi ya mechi husika ni muhimu kurejea kwenye njia wakati ujao na kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Nidhamu itaongeza utendaji mkubwa kwenye utendaji kazi katika mechi zilizopo kitaifa na kimataifa kwa kuwa kila timu inatambua namna ya kupata matokeo kwenye mechi ambazo watakuwa uwanjani.

Wachezaji ni muda wa ufanya kazi kwa juhudi uwanjani ili kuwapa furaha mashabiki na kutimiza majukumu kwa wakati pale mtakapopata majukumu.

Kila mmoja afanye kazi kwa umakini ili kuongeza ushindani kwenye ligi na mechi za kimataifa. Kwa upande wa waamuzi ni wakati wa kuendelea kufuata sheria 17 za mpira kupunguza malalamiko kabisa.

Previous articleTABORA UNITED WATANGAZIWA JAMBO HILI NA YANGA
Next articleKAZI NZITO LEO HAPA LIVERPOOL PALE ARSENAL