Home Uncategorized SIMBA YAPOTEZA KARIAKOO DABI

SIMBA YAPOTEZA KARIAKOO DABI

KATIKA mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Desemba 22 ubao ulisoma Simba 0-4 Yanga kwenye NBC Premier League.

Simba wakiwa wenyeji walishuhudia wakifungwa dakika ya 16 kupitia kwa Willyson Christopher, Shaban Ibrahim dakika 23, Ahmed Denis dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti, Hemed dakika ya 58.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally baada ya matokeo hayo ameweka wazi kuwa hayajawa matokeo mazuri lakini ni somo kwa ajili ya kufanya vizuri kesho.

“Matokeo hayajawa mazuri lakini niwape pole wachezaji na mashabiki. Bado kuna mpango mzuri kwa ajili ya kuwa na timu imara huu ni mwanzo tunaamini tutafanya vizuri wakati ujao,”.

Previous articleAMEACHA BALAA HUKO CAF PACOME/MUDA
Next articleTABORA UNITED WATANGAZIWA JAMBO HILI NA YANGA