Home Uncategorized SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KMC

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KMC

BENCHI la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa litaingia kwa tahadhari kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Simba ilitoka kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao uliopita wa ligi ambapo mabao yalifungwa na Saido Ntibanozkia, Sadio anoute na John Bocco.

Leo inakutana na KMC  ambayo yenyewe kwenye mchezo wake uliopita iligawana pointi mojamoja dhidi ya Singida Fountain Gate.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua ubora wa wapinzani wao KMC hivyo wataingia kwa tahadhari kupata matokeo chanya.

Tunatambua uimara wa KMC ambapo kila tunapokutana mechi yetu haijawahi kuwa rahisi.Ni mbinu ambazo tutazitumia kuwakabili tunaamini zitatupa matokeo chanya kutokana na wachezaji kuwa tayari kutafuta pointi tatu,” .

Ni Ahamid Moalin anakinoa kikosi cha KMC ameweka wazi kuwa wapo tayari kuwakabili wapinzani wao kwenye mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa.

Simba baada ya kucheza mechi 9 ina pointi 22 ikiwa nafasi ya tatu inakutana na KMC yenye pointi 20 baada ya kucheza 13.

Previous articleKAZI NZITO LEO HAPA LIVERPOOL PALE ARSENAL
Next articleKMC YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA SIMBA