Home Uncategorized KMC YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA SIMBA

KMC YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA SIMBA

UBAO wa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 umesoma KMC 2-2 Simba na kuwafanya wababe hawa wagawane pointi mojamoja.

Katika mchezo wa leo KMC walianza kwa kuchukua tahadhari kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza walipata bao la kuongoza dakika 30 kupitia kwa Wazir Junior aliyefunga bao la pili pia dakika ya 88.

Kwa Simba ni Saido Ntibanzokiza dakika ya 57 alipachika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Jean Baleke.

Ayoub Lakred kipa wa Simba leo jitihada zake za kuokoa hatari langoni zimegonga mwamba akitunguliwa mabao yote mawili na Wazir aliyekuwa kwenye ubora wake ndani ya dakika 90 za mchezo wa leo.

Previous articleSIMBA YATUMA UJUMBE HUU KMC
Next articleYANGA WANA BALAA HAO, AZIZI KI HASHIKIKI