KAMATI ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeufungia Uwanja wa Liti, uliopo Singida.
Uwanja huo ambao unatumiwa na Singida Fountain Gate kwa mechi za nyumbani kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara sasa hautatumika kwa michezo ya ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Taarifa ya kamati hiyo inasema eneo la kuchezea (pitch) la uwanja huo halifai kuchezewa mpira kutokana na eneo hilo kutokuwa na nyasi kijani kwa sehemu kubwa.