Home Uncategorized MITAMBO YA MABAO SIMBA YAREJEA

MITAMBO YA MABAO SIMBA YAREJEA

MITAMBO ya mabao ndani ya kikosi cha Simba imerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti tayari kuwakabili Tanzania Prisons, kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ni Jean Baleke mshambuliaji namba moja ndani ya Simba akiwa na mabao matano pamoja na Luis Miquissone kiungo mwenye pasi moja aliyotoa kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Baleke alipata maumivu ya mguu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na nahodha John Bocco, Luis hakuwepo mazima katika kikosi hicho.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wao wanaendelea na maandalizi kwa mechi za ushindani.

“Kuhusu Jean Baleke alipata maumivu kwenye mguu kidogo lakini alipewa huduma na kurejea kwenye utimamu hata kwenye mazoezi ya timu yupo.

“Luis Miquissone hakuwepo kabisa kwenye mchezo wetu dhidi ya Power Dynamos kutokana na kutokuwa fiti lakini kwa sasa anaendelea vizuri yupo tayari kuelekea mchezo wetu ujao dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba inatarajiwa kutupa kete yake ya nne kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Sokoine, Oktoba 5.

Previous articleMPIRA SIO VITA, AFYA NA UMAKINI NI MUHIMU
Next articleTANZANIA PRISONS YAZITAKA POINTI ZA MNYAMA