Home Sports MPIRA SIO VITA, AFYA NA UMAKINI NI MUHIMU

MPIRA SIO VITA, AFYA NA UMAKINI NI MUHIMU

MWENDO wa Ligi Kuu Bara unazidi kupasua anga taratibu. Tunaona namna ambavyo kazi kubwa ipo kwenye msako wa pointi tatu muhimu hili ni jambo la msingi.

Pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wanajituma kutimiza majukumu yao. Kila mmoja anapenda kuona namna ilivyo mwisho wa mchezo muhimu kuwa makini kwenye kutafuta ushindi.

Mzunguko wa tatu umekwenda na mzunguko wa nne kila timu inapambana kuonyesha uwezo. Wachezaji katika kutimiza majukumu matumizi ya nguvu yanazidi kuwa makubwa zaidi.

Katika mechi ya Dodoma Jiji dhidi ya Azam FC tumeshuhudia namna kazi kubwa ilivyofanyika. Haina maana kwamba matumizi ya nguvu hayatakiwi hapana jambo la msingi ni umakini kwenye mchezo husika.

Ni dakika 90 za jasho kwa wanaume kupambana na mwisho hakuna ambaye alikuwa mbabe. Kugawana pointi mojamoja ilikuwa ni halali yao kwenye mchezo huo.

Ulikuwa ni moja ya mchezo uliokuwa na matumizi makubwa ya nguvu na upotevu wa muda bila hesabu. Tuache mpira utembee kwenye njia zake na mbinu za walimu ziamue matokeo.

Mchezo wa Simba dhidi ya Coastal Union haukuwa na matumizi makubwa ya nguvu ila umakini ulikosekana na mwisho mchezaji Henock Inonga aliumia.

Mzunguko wa tatu , nne mpaka mwisho wa ligi haitapendeza kucheza mpira kama vita, mpira ni burudani wachezaji ni muhimu kutambua hilo.

Hata mchezo wa Yanga na Namungo bado kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu, muhimu kuongeza umakini kila wakati.

Burudani inapaswa itolewe kwa mashabiki na wachezaji wawe na furaha katika kutimiza majukumu yao.Hili suala la matumizi ya nguvu mahali pasipotakiwa ni muhimu kuliweka kando.

Previous articleBAADA YA KUPOTEZA, YANGA WAJA NA TAMKO HILI
Next articleMITAMBO YA MABAO SIMBA YAREJEA