Home Sports AZAM FC WANA BALAA HAO, SIMBA TATIZO

AZAM FC WANA BALAA HAO, SIMBA TATIZO

WAKATI ikiwa ni saa kadhaa zinahesabika kufika mchezo wa Mzizima Dabi, Uwanja w Mkapa, rekodi zinaonyesha kuwa Azam FC wana balaa kwenye eneo la ushambuliaji kutokana na kasi yao kuwa hivyo.

Msimu wa 2023/24 haujawa bora kwa Simba katika eneo la ushambuliaji kutokana na aina ya washambuliaji waliopo kukosa nafasi wanazozipata kwenye mechi zao.

Kinara wa utupiaji ni Saido Ntibanzokiza na Clatous Chama ambao wote wawili wametupia mabao 7 ndani ya ligi huku Chama yeye atakosekana kwenye mchezo kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

Safu ya ushambuliaji ya Azam FC imetupia jumla ya mabao 52 ikiwa ni namba mbili kwa timu zenye mabao mengi ndani ya msimu wa 2023/24. Namba moja kwenye utupiaji ni Yanga wenye mabao 57.

Azam FC inawakaribisha Simba ambayo ni namba tatu kwa timu zenye mabao mengi ambapo ni mabao 47 yamefungwa na timu hiyo ambayo kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu.

Kazi kubwa itakuwa kwa wababe hao kusaka pointi tatu baada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kutoshana nguvu kwa kumalisha dakika 90 ubao ukisoma Simba 1-1 Azam FC.

 Tatizo kubwa kwa Simba ndani ya tatu bora ikiwa ni namba moja kwa timu iliyoruhusu mabao mengi kwa msimu wa 2023/24. Licha ya kucheza mechi 24 huku  Azam FC ikiwa  imecheza mechi 25 bado Simba ni namba moja katika kuruhusu mabao.

Ukuta wa Simba umeruhusu jumla ya mabao 23 wakikusanya pointi 53 kibindoni ndani ya ligi. Namba moja kwa kuruhusu mabao machache ni Yanga iliyokusanya jumla ya mabao 12 inafuatiwa na Azam FC iliyoruhusu mabao 16.

Mkali wa kucheka na nyavu Azam FC ni kiungo mshambuliaji Feisal Salum mwenye mabao 15 na pasi sita za mabao.

Previous articleREAL MADRID IMETINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Next articleAZIZ KI AMECHANGANYA KINOMA