Home Sports YANGA YASEPA NA TATU ZA KAGERA SUGAR, MUDA KAFANYA YAKE

YANGA YASEPA NA TATU ZA KAGERA SUGAR, MUDA KAFANYA YAKE

YANGA imesepa na pointi tatu za Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Bao pekee la ushindi limefungwa na kiungo mshambuliaji Mudathir Yahya dakika ya 83 akitumia pasi ya Aziz KI kiungo wa Yanga ambaye anafikisha pasi 8 za mabao.

Yanga ni pointi 68 wanafikisha ndani ya ligi wakiwa namba moja kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo wa leo Kagera Sugar walitumia mbinu ya kujilinda zaidi mwanzo mwisho nafasi waliyompa Muda ambaye alianzia benchi ilitosha kuwaadhabibu.

Ipo wazi kwamba Yanga wanakaribia kutwaa taji la ligi kwa msimu wa 223/24 ambapo litakuwa ni la 30 kwao.

Previous article40 IMPERIAL CROWN KASINO, UTAJIRI KWA TAJI LA MERIDIANBET
Next articleCHEZA KASINO YA MOON OF THOTH, HISTORIA YA MISRI YA KALE ILIPO