Home Uncategorized HIKI HAPA KINACHOMBEBA JEZI NAMBA SABA WA YANGA

HIKI HAPA KINACHOMBEBA JEZI NAMBA SABA WA YANGA

NYOTA wa Yanga, Maxi Nzengeli amesema kuwa kinachombeba ndani ya kikosi hicho kuwa kwenye ubora ni ushirikiano ambao anapata kutoka kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Ndani ya kikosi cha Yanga yeye anavaa jezi namba saba mgongoni akiwa na uwezo wa kupanda na kushuka kwenye kutimiza majukumu yake.

Nzengeli amepenya kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi akiwa ameshaanza kuonyesha makeke yake ya kufunga ndani ya ligi.

Ni mabao mawili kafunga ilikuwa mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex akiwa ametoa pasi moja ya bao.

Nzengeli amesema: “Furaha kubwa ninapopata nafasi ya kucheza na wachezaji wakinipa ushirikiano hili ni jambo kubwa ambalo ninafurahia ninawashukuru wao pamoja na benchi la ufundi.

“Mashabiki wanaonesha mapokezi makubwa tukiwa uwanjani tunafurahi uwepo wao. Wazidi kuwa pamoja nasi kwani bado tunaendelea na kazi na mechi za kucheza zipo nyingi,” .

Yanga ni namba moja kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi mbili msimu wa 2023/24.

Previous articleHAWA HAPA WAMEBEBSHWA KAZI NA KOCHA SIMBA
Next articleMAXI APIGWA STOP YANGA, SIMBA SC TUNATOBOA CAF