HAWA HAPA WAMEBEBSHWA KAZI NA KOCHA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewaambia wachezaji wake wapya kuwa sasa ni muda wao muafaka wa kuonyesha thamani yao katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inatarajiwa kuanzia ugenini nchini Zambia dhidi ya Power Dynamos katika hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa Septemba 15, mwaka huu.

Kikosi hicho tayari kipo kambini tangu  Jumanne kikijiandaa na mchezo huo wa kimataifa ambacho kitaongozwa na nyota wapya baadhi Willy Onana, Luis Miquissone, Fondoh Che Malone na Aubin Kramo.

 Robertinho amesema kuwa anaamini ubora wa wachezaji hao wapya wataipa matokeo mazuri katika mchezo huo wa kwanza wataoacheza ugenini.

Robertinho amesema ni muda wa wachezaji hao kuonyesha kile ambacho kimewaleta, Simba kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ya uwanjani kwa kuonyesha kiwango bora sambamba na burudani ya soka.

“Ni muda wa wachezaji wangu wapya kuonyesha thamani ya uwanjani kwa mashabiki wao, kwa kucheza soka safi la pasi kwa lengo la kuwapa burudani mashabiki na ushindi.

“Ninafahamu uwezo wa kila mchezaji wangu, ni muda wao kuwaonyeshea mashabiki kuwa kipi kimewaleta hapa Simba katika msimu huuu.

“Kila mchezaji anafahamu malengo ya timu msimu huu ambayo ni kufika hatua ya nusu fainali, hivyo kila mchezaji atakayepata nafasi ya kucheza ni lazima atoe mchango” amesema Robertinho.