HUYO KRAMO ANA BALAA KWELI HUKO
AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa nyota wao Aubin Kramo ana balaa akiwa kwenye uwanja wa mazoezi jambo linaloongeza nguvu kwenye kikosi hicho. Nyota huyo aliyeibuka Simba akitokea ASEC Mimosas hajaonyesha makeke yake uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeraha alipopata maumivu wakati wa maandalizi ya Ngao ya Jamii, Mkwakwani,…