Home Sports WINGA KUTOKA JANGWANI MIKONONI MWA DODOMA JIJI

WINGA KUTOKA JANGWANI MIKONONI MWA DODOMA JIJI

BAADA ya kupewa mkono wa asante ndani ya kikosi cha Yanga winga Dickson Ambundo kuna uwezekano mkubwa akarejea katika kikosi cha Dodoma Jiji.

Ambundo anaingia kwenye rekodi ya kuwa mzawa aliyeingia kwenye orodha ya wachezaji waliofika katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea nafasi ya pili.

Pia akiwa Yanga ni miongoni mwa waliotwaa mataji ya ligi mara mbili ikiwa ni msimu wake wa kwanza 2021/22 na 2022/23 baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Dodoma Jiji.

Taarifa zinaeleza kuwa Dodoma Jiji wapo kwenye mpango wa kufanya maboresho kwenye kikosi hicho na miongoni mwa nyota wanaotajwa ni pamoja na Ambundo kutoka Yanga.

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2022/23 Ambundo akiwa na uzi wa Yanga alicheza mechi 13 na kukomba dakika 454 alitoa pasi moja ya bao.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa mipango iko poa.

“Kuhusu usajili wa nani atakuja ama nani ataondoka ni ripoti ya benchi la ufundi itasema hivyo ni jambo la kusubiri na kuona,”.

Previous articleUSAJILI SIMBA WAVUJA
Next articleKIRAKA WA KAZI KUTOKA MSIMBAZI MALI YA NAMUNGO FC