Home Sports HAWA HAPA WANAOTAKIWA MKUTANO MKUU YANGA

HAWA HAPA WANAOTAKIWA MKUTANO MKUU YANGA

IKIWA imekamilisha msimu wa 2022/23 na mataji mkononi kesho Juni 24 Wanachama wa Yanga wanatarajiwa kufanya mkutano mkuu.

Yanga imetwaa mataji yote iliyokuwa inapambania kwenye ardhi ya Bongo ikiwa ni pamoja na Ngao ya Jamii, ligi na Kombe la Azam Sports Federation.

Kwenye anga la kimataifa Yanga katika Kombe la Shirikisho Afrika imegotea nafasi ya pili baada ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya USM Alger.

Kwa mujibu wa ibara ya 17(1) ya katiba wanaotakiwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Wanachama utakaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) Dar es Salaam ni;

1. Mwenyekiti wa tawi
2. Katibu wa tawi
3. Mwekahazina
4. Wajumbe wawili wa mkutano mkuu kutoka kwenye tawi.

Previous articleLEGEND MKUDE, NYONI THANK YOU HAZIWATOSHI
Next articleUSAJILI SIMBA WAVUJA