Home Uncategorized KOCHA YANGA:MAYELE ATAKUWA MFUNGAJI BORA

KOCHA YANGA:MAYELE ATAKUWA MFUNGAJI BORA

MWINYI Zahera aliyewahi kuifundisha Yanga na kwa sasa akiwa ndani ya Polisi Tanzania ameweka wazi kuwa anaona tuzo ya mfungaji bora ikienda kwa Fiston Mayele.

Zahera alikuwa benchi Juni 6, 2023 aliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Simba 6-1 Polisi Tanzania huku Saido Ntibanzokiza akitupia mabao matano na bao moja likifungwa na Israel Mwenda.

Ntibanzokiza anafikisha jumla ya mabao 15 kibindoni akiwa tofauti ya bao moja na mshambuliaji Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 kibindoni.

Kocha huyo amesema kuwa kukosa kwake msimu uliopita tuzo ya ufungaji bora kulimpa hasira jambo lililofanya apambane kwa wakati mwingine kushinda.

“Naona kilichotokea msimu uliopita alipokosa tuzo ya ufungaji bora kulimpa hasira na kumfanya apambane kufanya vizuri kwenye ligi na kimataifa kwa hali ilivyo bado ninaona ana nafasi ya kutwaa tuzo ya ufungaji bora.

“Hakuna ambaye alijua kwamba Saido atafunga mabao aliyotufunga , (matano) na wote wamebakiwa na mchezo mmoja. Mpira ulivyo Mayele anaweza akapewa nafasi mchezo ujao na Saido naye akapewa nafasi mchezo ujao wote wakashindwa kufunga.

“Hivyo tusubiri na tuone mchezo wa mwisho utaamua nani atakuwa ila siwezi kusema kuwa Saido hawezi kuwa mfungaji bora wala siwezi kusema kwamba Mayele hatakuwa mfungaji bora,” .

Previous articleSIMBA: NTIBANZOKIZA ATAKUWA MFUNGAJI BORA
Next articleSURE BOY KAIBUKIA MBEYA