Home Uncategorized YANGA KUREJEA KIMATAIFA WAKIWA IMARA

YANGA KUREJEA KIMATAIFA WAKIWA IMARA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utarejea kwenye mashindano ya kimataifa wakati mwingine ukiwa imara zaidi.

Timu hiyo kutoka Tanzania imeandika rekodi nzuri ya kucheza fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni ya kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.

Imegotea kuwa mshindi wa pili baada ya ushindi wa jumla ya Yanga 2-2 USM Alger kuwabeba Waarabu wa Algeria ambao walishuhudia Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 1-2 USM Alger.

Ugenini ubao ulisoma USM Alger 0-1 Yanga hivyo kila timu imeshinda ugenini lakini kwa wapinzani wa Yanga wamefaidika na ushindi wa ugenini.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamvaa medali ndani ya Yanga ni pamoja na mzee wa kuchetua Bernard Morrison, Fiston Mayele mkali wa kucheka na nyavu, Dickson Job na Farid Mussa.

Kikosi hicho tayari kimewasili Dar na leo Juni 5 kimepewa mualiko Ikulu kwa ajili ya pongezi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa walipofikia ni jambo la kushuruku na wanaamini watarejea wakiwa bora kwa wakati ujao kwenye mashindano ya kimataifa.

“Tulikuwa na malengo ya kutwaa ubingwa lakini imeshindikana, pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki kwa namna walivyokuwa pamoja nasi.

“Serikali kila hatua ilikuwa pamoja nasi hivyo tunaamini kwamba tutarejea tukiwa imara wakati ujao,”.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
Next articleKOCHA SIMBA AMKOMALIA ONYANGO